Thursday, 3 September 2015

Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea
1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa
kutujali uzima.
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha
upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia
ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa
sio uadai.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya
upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na
hakuna aliyenipa likizo yoyote.
7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na
siasa tangu 28.7.2015 saa sita usiku baada ya
kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani
ya chama changu.
8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA
Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo
ilitufanya
tusielewane.
9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma,
Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa
alinipigia simu
kutaka kujua nii cha kufanya.
10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na
tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.
11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo
wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza
atangaze
kuhama chama, aweke wazi ni chama gani
anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake
12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza
kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma
zake, kitu
kilichonifanye nitofautiane naye.
13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa
Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?
14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha,
mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo
na sifa
ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa
ya urais kama watu wanavyosema
15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa
Lowassa, Swali langu la Lowasssa kuwa Mtaji au
mzigo
halikuwahi kujibiwa.
16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja
nao na ni viongozi gan atakuja nao.
17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa
CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa
wilaya.
18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe
majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july
sikupewa hayo majina
19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27
niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa
sababu ,