Sunday, 25 September 2016

Rihanna kuja Tanzania

Rihanna anapenda watoto waende shule. Taasisi yake ya Clara Lionel Foundation imeungana na Global Partnership for Education and Global Citizen katika mradi wa miaka mingi wa kusaidia elimu duniani.




Kupitia mradi huu, Rihanna ana matumaini ya kuwatetea watoto zaidi ya robo bilioni ambao hawapo shuleni pamoja na wanafunzi milioni 330 ambao hawajifunzi kitu katika shule walizopo.


Akiwa kama balozi mpya wa dunia wa GPE, Rihanna anatarajiwa kufika katika nchi zinazoendelea zaidi ya 60, akizipa kipaumbele zile zenye uhitaji zaidi zikiwemo zenye migogoro. Tanzania ni moja kati ya nchini zenye changamoto kubwa za elimu.

Mwenyekiti wa GPE, waziri mkuu wa zamani wa Australia, Julia Gillard amesema anayo furaha kubwa kuingia ushirikiano na Rihanna, ambaye jina lake halisi ni Robyn Fenty.

Rihanna alianzisha Clara Lionel Foundation mwaka 2012 kwa kumbukumbu ya bibi na babu yake, Clara na Lionel Braithwaite

Amber Lulu avujisha picha zake za utupu

Model na video queen wa  muziki wa bongo fleva

Kama inde ya prince dully Sykes na Harmonize   maarufu  kwa jina Kama amber lulu , ameweka picha  zinaonyesha umbile lake akiwa mtupu katika ukurasa wake wa Instagram.

Friday, 2 September 2016

Diamond na kevin hart

Mwimbaji wa bongofleva Diamond Platnumz yuko Marekani kwaajili ya kufanya show Los Angeles September 2 lakini pia kufanya video ya kolabo yake na Neyo ambapo kwenye pitapita zake kakutana na Kevin Hart.

Kevin Hart ameonekana kumpokea vizuri Diamond na hata kwenye video Diamond aliyorekodi mchekeshaji huyu alisalimia Tanzania na kumalizia na utani wa utambulisho wa jina lake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kukutana na mastaa wa dunia kwenye safari zake za Marekani, amekutana nao kadhaa akiwemo Nelly na Kanye West, tazama hii video fupi hapa chini.