Monday, 1 August 2016

Desiigner ataja kiasi alichonunua beat ya ‘Panda’

Rapper wa Marekani Desiinger ambaye anafanya vizuri na single yake ya ‘Panda’, hivi karibuni alisema aliununua mdundo wa wimbo huo kwa kiasi cha dola $200 ambayo ni kama laki nne na nusu hivi za kibongo.



 Desiinger anasema, “Nilikuwa gheto na washkaji zangu tukivuta bangi tu ndani ya nyumba huku tukicheza GTA [Grand Theft Auto] mara mshkaji wangu akapiga wimbo kutoka kwenye computer na kuniuliza kama naweza kuandika kitu kwenye mdundo huo nikamwambia naweza nikafanya hivyo, beat hiyo ilikuwa Youtube tu na baada ya siku mbili nikautoa wimbo huo.”

​No trouble in paradise: Zari azipuuzia tetesi zinazozidi kuvuma kuhusu kusalitiwa na Diamond

Trouble in paradise? Kwa tetesi zinazozidi kuvuma kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhusiano wa couple yenye nguvu zaidi Afrika Mashariki, Diamond na Zari, jibu linaweza kuwa ndiyo!

Lakini huenda tetesi hizo zikaendelea kuishia tu Instagram kwasababu wawili hao hawaoneshi dalili za kuyapoteza mahaba mazito kati yao.
Zari alithibitisha kupitia Snapchat kuwa yeye na mpenzi wake, hitmaker wa Kidogo, Diamond wanatarajia mtoto wa pili – wa kiume, lakini tetesi za usaliti zimeendelea kuwawinda kila kukicha.
Wikiendi hii kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii inayomuonesha Hamisa Mobetto akiwa kwenye chumba cha hoteli kinachofanana kwa kiasi kikubwa na chumba ambacho Diamond alionekana akiwemo katika video aliyoiweka Instagram inayomuonesha akiuimba wimbo wake Kidogo aliowashirikisha P-Square.
.


Ni katika chumba hicho pia staa huyo alikitumia akiwa na Zari.
Picha hiyo imesababisha mjadala mkubwa wikiendi yote, huku baadhi ya mashabiki wakimshambulia Hamisa kwa kile wanachoamini anaweza kuwa sababu kubwa ya kusababisha mtafaruku katika uhusiano huo, wengine wakimuonea huruma Zari kuwa kama yasemwayo ni kweli basi hatendewi haki na mpenzi na wengine wakimshambulia Diamond kwa kuhisi anamkosea heshima mwanamke ambaye si tu amemzalia mtoto mrembo wa kike, Tiffah, bali pia yu mbioni kumbariki kwa mtoto mwingine wa kiume.
Hata hivyo mambo yako tofauti kwa Zari ambaye post zake za Instagram na Snapchat zinatuma ujumbe mwingine – positive vibes only. Kwenye moja ya post za Snapchat, staa huyo wa Uganda anaonekana akiwa kwenye mgahawa wa kifahari huku akiionesha pete ya thamani kwenye kidole chake cha chanda.
Pia kwenye Instagram amepost picha na kupeleka ujumbe huo huo – no trouble in paradise









Justin Bieber aikataa ofa ya $5m kutumbuiza kwenye show ya chama cha Republican

Justin Bieber amemfanyia kitu mbaya Donald Trump.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, staa huyo alikataa kuchukua dola milioni 5 alizopewa ili atumbuize kwenye show ya chama cha Republican wakati wa mkutano wake wa hivi karibuni huko Cleveland, Marekani.
Vyanzo vimedai kuwa mchezaji wa kikapu,  LeBron James pamoja na meneja wa Bieber, Scooter Braun ni watu waliomshawishi aikatae ofa hiyo.
James alimkataza Bieber kutumbuiza huku Braun akimtishia kujiondoa kama meneja wake iwapo angekubali.
CAA, kampuni inayomwakilisha Bieber, ilipokea ofa hiyo. Ilikuwa ni ya kutumbuiza kwa dakika 45 kwenye ukumbi karibu na Quicken Loans Arena, ambako mkutano mkuu wa Republican ulifanyika.
Japo mapromota hao walidai kuwa show hiyo haikuwa ya kisiasa, kiasi hicho cha fedha kilichangwa na wadhamini wa chama hicho.
Kiasi hicho cha fedha kingekuwa malipo makubwa zaidi ya mara moja kwa Bieber kupewa katika maisha yake ya muziki, au kikubwa zaidi kwa msanii kuwahi kupewa mara moja.
Awali Bieber alikuwa amefikiria kutumbuiza kutokana na kuwa na asili na Canada na kwamba siasa ya Marekani haimhusu.
Hata hivyo meneja wake ni shabiki mkubwa wa mgombea Urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na pia mmoja wa wachangishaji fedha.
Inasemekana kuwa awali Braun alishauri Bieber atumbuize huku kukiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Black Lives Matter’ kwenye show hiyo.
Mapromota hao walikaa wazo hilo na kupendekeza mabango yaandikwe ‘All Lives Matter.’ Mapromota hao pia walimkataza Bieber asiseme kitu chochote kibaya kumhusu Trump au chama chake. Matokeo yake, Braun alisema asingemwakilisha tena Bieber kama angechukua ofa hiyo.
Ingawa mapromota walimweleza Scooter kuwa LeBron James angekuwepo kwenye tukio hilo huko Cleveland wiki hiyo kuwakaribisha wanasiasa bila kuwa na msimamo wa kisiasa, James alidaiwa kukataa na kumtaka Bieber naye aitose ofa hiyo.
Bendi ya Bieber pia ilikuwa na ushawishi na uamuzi wake. Kwa mujibu wa ripoti, kila member wa bendi hiyo ni mweusi na kila mmoja aliipinga show hiyo.
Mwishowe, Bieber akawa hana ujanja zaidi ya kuikataa ofa hiyo