Tuesday, 31 May 2016

Tyga na Kylie

MAPENZI BILA PESA, WAPIII, KYLIE JENNER
KAFUNGUKA KUHUSU KUMKOPESHA TYGA
DOLA MILIONI 2

Staa wa tv Kylie Jenner amekanusha kuwahi
kumkopa Ex wake Tyga dola milioni $2 na
kwamba kwa sasa hana pesa ndio maana anamdai
rapa huyu.

Kupitia twitter Kylie amesema stori hizi ni za
uongo na kwamba hajawahi kumpa dola milioni
mbili Tyga,Tyga amekuwa miongoni mwa rapa
waliotajwa kutokuwa na pesa nyingi hata kama
anaishi maisha ya kistaa.

Hivi karibuni baada ya kuachana na Kylie, Tyga
ametajwa kuanzisha mahusiano na
mwanamitindo kutoka Uingereza Demi Rose.
Tyga kwa sasa ana record mpya kwenye radio
inaitwa #Cash_Money

Wolper ajibu madai ya kufilisiwa na mkongo

Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper baada ya kukiri kwamba anatoka kimapenzi na Harmonize, amefunguka na kueleza madai ya kufilisiwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani.


Akiongea katika promo ya kipindi kipya cha Take One ambacho kinatarajiwa kuruka Jumanne hii, Wolper amedai yeye ndiye aliyetendwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake, kwani wakati anaanza naye mahusiano alikuwa ana gari na nyumba lakini baadae akijikuta hana hata sehemu yakulala.

Muigizaji huyo ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika filamu zake, amedai alikuwa anajilipia nyumba kwa dola, lakini ulifikia wakati akafilisika na kuanza kulala hoteli.

Wolper amedai mahusiano hayo yalimsababishia kugombana na baadhi ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wakimshauri vizuri, lakini yeye alikuwa akiwaaona kama wanamfitini.

Muigizaji huyo ambaye amewahi kutamba na filamu yake Tom Boy, kwa sasa anatoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’, Harmonize kutoka WCB.

Monday, 30 May 2016

Sikiliza nyimbo hii mpya ya Rich Mozilah-Tupendane

Pakua nyimbo ya msanii mpya wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo cha .UDSM, Rich Mozilah na nyimbo yake inayoitwa "TUPENDANE"
Gusa link hii ili kupakua,
http http://mdundo.com/a/16670


Monday, 23 May 2016

Kampuni ya MOSAN inatangaza nafasi za kazi

KAMPUNI YA MOSAN LIMITED INAKUTANGAZIA NAFASI ZA KAZI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:
1.       MAAFISA MASOKO NA MAUZO (SALES AND MARKETING OFFICERS)
2.       MAAFISA MAUZO (SALES OFFICERS)

SIFA
I.                    UWEZO WA KUENDESHA PIKIPIKI NA GARI
II.                  UWEZO WA KUUZA NA KUTAFUTA MASOKO, PIA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIASHARA
III.                MAARIFA YA MASOKO
TUMA MAELEZO BINAFSI (CV) KWENYE EMAIL HII: employment.mosan@gmail.com.

AU PIGA SIMU HII KWA MAELEZO ZAIDI: +255 717 49 87 73.
Mwisho wa kutuma maombi ni Mei, 27, 2016.

Sunday, 22 May 2016

Manchester United kumtangaza Jose Mourinho

Manchester United wanatarajia kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya, BBC Sport imeripoti.



Inaaminika kuwa deal hiyo na raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 ilikubaliwa kabla ya ushindi wa United kwenye fainali ya kombe la FA dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.

Ikiwa United imeshindwa kufuzu kushiriki kombe la mabingwa wa Ulaya chini ya kocha wake wa sasa, Louis van Gaal, uongozi wa Old Trafford unafikiriwa kuamua kufanya mabadiliko yanayohitajika.

Mourinho amekuwa benchi tangu atimuliwe na Chelsea December mwaka jana.

Klabu hiyo imepanga kutangaza ujio wake mapema wiki ijayo baada ya kumwambia Van Gaal, 64, afungashe virago vyake.

Kocha huyo raia wa Uholanzi bado ana msimu mmoja kwenye mkataba wake wa miaka mitatu na licha ya kutumia paundi milioni 250 kusajili wachezaji wapya, ukocha wake umewaangusha mashabiki wengi kwa timu yake kumaliza katika nafasi ya nne na kisha ya tano kwenye ligi kuu ya England katika misimu miwili aliyoifundisha.

Mourinho alikuwa kwenye mchezo wa masumbwi Jumamosi hii ambapo bondia David Haye alishinda lakini alikataa kuongea chochote iwapo anaenda kumrithi Van Gaal.

Mourinho ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi huku akishinda vikombe vitatu akiwa na Chelsea, pamoja na kuingoza  Porto na Inter Milan kwenye ushindi wa ligi ya mabingwa mwaka 2004 na 2010.

Aliwahi pia kuwa kocha wa Real Madrid na kuiwezesha kushinda kombe la Spanish La Liga mwaka 2012.

Friday, 20 May 2016

Da Prince Mo kuachia kazi mpya hivi karibuni

 Da Prince Mo msanii wa mziki wa bongo fleva hivi karibuni ataachia nyimbo mpya nyimbo yake ya kwanza kufanya vizuri kwenye radio na tv stations


Mashabiki wake wakae tayari kwa kupokea kazi hiyo kwa kufuatilia katika social networks zake 
Facebook : Da Prince Mo
Instagram @Daprincemotz

Sunday, 15 May 2016

Neyo na Diamond kushusha bonge la show Mwanza jumamosi

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul”Diamond Platinum’s”akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na jinsi atakavyoshiriki kutoa burudani na kuimba wimbo wa pamoja na mwanamuzi NE-YO wa nchini Marekani katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016,litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege,Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania.

Moto wa burudani utawaka katika jiji la Mwanza  Jumamosi ya wiki ijayo ambapo msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva kutoka Marekani NE-YO atakapo shusha bonge ya shoo  kwa kushirikiana na wasanii wa hapa nchini katika uwanja wa CCM Kirumba kwenye  onyesho lililotayarishwa na Jembe Media chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.

Akiongea juu ya onyesho hilo la kihistoria katika ukanda wa ziwa Magharibi,Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa  Vodacom inayo furaha kudhamini tamasha hili kubwa litakaloleta burudani ya muziki kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Aliwataja baadhi ya wanamuziki watakaowasha moto kumsindikiza NE-YO  kuwa ni  Diamond,Ney wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma Nature,Mr.Blue,Stamina,JJ Bendi na wengineo .

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe  ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt.Sebastian Ndege  aliwataka wapenzi wa muziki kujitokeza kupata budurani ya mwaka katika tamasha hilo na mipango ya tamasha hilo kubwa imekamilika na kuwataka wapenzi wa muziki wa Mkoa wa Mwanza wakae mkao wa kula wa  ya karne.

Kuhusiana na viingilio alisema kuwa tiketi zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na kuongeza kuwa wanamuziki watakaoshiriki onyesho hili wamejipanga kutoa burudani kisawasawa na kukata kiu ya wapenzi wa muziki wote Nchini.

Alisema tiketi za onyesho hilo zitauzwa katika vituo mbalimbali Nchini yakiwepo maduka ya Vodacom Tanzania,Pia zitapatikana  kupitia huduma ya M-Pesa,Katika kuwapunguzia washabiki usumbufu wa kupanga misururu ya kununua tiketi za onyesho hilo pia zitauzwa kwa kupitia huduma ya M-Pesa bila kuwepo na makato yoyote ya kutumia huduma hiyo ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo kutakuwepo na utaratibu maalumu wa kuingia kwenye onyesho cha muhimu ni kutunza namba zao za kumbukumbu ya mhamala wa malipo.Jinsi ya kujipatia tiketi kwa njia ya M-PESA mteja anatakiwa kupiga  *150*00# na kuchagua LIPA KWA M-PESA
2.       Chagua MANUNUZI
3.       Chagua JEMBEKA FESTIVAL
4.       Weka namba ya kumbukumbu – 200200
5.       Weka kiasi – 10,000
6.       Weka Namba yako ya siri  na kwa wale wa tiketi za VIP namba ya kumbukumbu ni 200100 bila malipo yeyote yale.
v Kwa msaada wa kununua tiketi, piga BURE namba 0800 71 0040

Alikiba afafanua kwanini M.I hayupo kwenye video ya Aje

audio ambayo ilisambaa wiki hii ikiwa na sauti ya rapper huyo ni demo (ilikuwa haijakamilika). “Tulivyokuwa tumeplan kufanya video na nini ratiba za M.I zilikuwa zipo tight na mimi sikutakiwa kuendelea kuchelewa sababu muda ulikuwa umeenda,” amesema Kiba.

“Kulikuwa na Plan B vilevile ndio nikaweza kufanya nyimbo nyingine, I mean nikaweza kurudia zile verse ambazo M.I alitakiwa afanye ila baada ya mimi kumaliza alituma ile nyimbo na tukaweza kuisikiliza lakini ilikuwa demo, kwahiyo tulikuwa nayo pending mpaka aweze kumaliza shughuli zake ndio tuweze kufanya video,” ameongeza.

“Lakini tukaona tunachelewa na kazi zilipokuwa nyingi, kila mtu ana ratiba zake na nyimbo ilikuwa ya kwangu kwahiyo tukaamua tufanye kitu tofauti, kama ulivyoona nimeimba French katika wimbo ambao nimetoa video yake.”

Dj Khhaled : nakuwa bubu kwa Beyonce

DJ Khaled anafahamika kwa kuwa mtu anayeongea sana lakini si pale anapokuwa mbele ya Beyonce.



Mkali huyo anazunguka na Queen Bey kwenye ziara yake ya Formation.

Ameliambia gazeti la The New York Times kuwa heshima aliyonayo kwa Bey ni kubwa mno kiasi cha kuwa muoga wa kuongea sana akiwa nay ili asije akaharibu.

“Nakuwa mkimya sana. Muda wote ambao nimewahi kuonana naye ni pale ninapokuwa na kaka yangu Jay Z, na huwa nasema “Hi,” na kuangalia upande mwingine haraka na ni kama nakimbia,” alisema.

“Sitaki tu kuongea sana. Siwezi nikaharibu.”

Thursday, 12 May 2016

Selena Gomez kwenye kashifa ya kuiba mume wa mtu

Selena Gomez amehusishwa kwenye mahusiano na Orlando Bloom baada ya kuonekana usiku wakiwa wote klabu baada ya show huko Las Vegas, nchini Marekani.



Ijumaa iliyopita Selena Gomez alifanya show kwenye ukumbi wa Mandalay Bay, Las Vegas lakini baadaye Orlando Bloom alihudhuria kwenye show hiyo kwa kushtukiza.



Orlando Bloom (39) ambaye ana mahusiano na Katy Perry, anahusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Selena Gomez (23) kutokana na picha zilizoonekana wakiwa wote baada ya show hiyo ya usiku wa Ijumaa.

Kwa taarifa za ndani zinadai kuwa Katy Perry ameamua kuachana na Orlando Bloom kutokana na picha hizo zilizosambaa mitandaoni.

Claudio Ranieri kateuliwa kuwa kocha bora wa mwaka

Kocha wa klabu ya Liecester City Claudio Ranieri achaguliwa kuwa kocha bora mwaka 2016 na kunyakuwa tuzo ya Enzo Bearzot inayotolewa na shirika la soccer nchini Italia.



Ranieri amejipatia tunzo hiyo baada ya kuisadia timu yake ya Leicester City kutoa ubingwa wa ligi ku ya Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo

Tuzo hizo zilianza kutolewa mwaka 2011 na shirika la soka Italia.

Wednesday, 11 May 2016

Shilole : mpenzi wangu ni hela tu

SHILOLE - MPENZI WANGU NI HELA

Uking’atwa na nyoka ukiguswa na jani lazima utaruka.
Baada ya kuvunjika kwa mahusiano na Nuh Mziwanda,
taarifa za chini zimezidi kuenea kuwa Shilole ana mahusiano
ya kimapenzi na msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nerd aliye
chini ya label ya Ommy Dimpoz, PKP.

Akiongea kwenye kipindi cha Busati, kinachoruka kupitia
Magic FM, Shilole amesema hana mpenzi kwa sasa.
.
“Mimi mpenzi wangu ni hela, Nerd ni rafiki yangu. Ukiwa
kwenye mapenzi unakuwa kama kipofu unakuwa hauoni.
Ukimkabidhi mtu moyo wako anakuwa anaufinyanga, kwa
sasa moyo wangu umestawi tofauti na zamani,” aliongeza.

Hata hivyo Shilole amesema hana namba ya Nuh Mziwanda
na hajawahi kuwasiliana naye tangu walipoachana. Kwa sasa
muimbaji huyo ana wimbo mpya uitwao Say My Name.

Harmonize kakataa kwamba anacopy style ya diamond

HARMONIZE: SIKOPI UIMBAJI WA DIAMOND

Harmonize amedai kuwa hamkopi bosi wake Diamond katika
uimbaji wake.

Hitmaker huyo wa Bado amedai kuwa Diamond ana
utambulisho wake hasa katika nyimbo za kulalamika na
kwamba huu ni muda sasa watu wakaanza kuwatofautisha.
.
“Ukimzungumzia Diamond unamzungumzia mtu ambaye ana
melody za malalamiko ambazo zimeganda katika vichwa vya
watu wengi, kwahiyo nikiimba malalamiko lazima watu
watakufafanisha,” Harmonize aliiambia 255 kupitia kipindi cha
XXL cha Clouds FM.
.
“Lakini huu ndio wakati mzuri wa kutambua huyu ni
Harmonize, huyu ni Diamond,” ameongeza.

Harmonize alimshirikisha bosi wake huyo kwenye wimbo
wake Bado unaofanya vizuri kwa sasa.

Beyonce afanya police waandamane

Kundi moja la maafisa wa polisi limefanya maandamano karibu na tamasha lililofanyika katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki Beyonce huko Houston.



Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo. Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.

Mwanamuziki huyo tayari amesema kwamba hawakosoi polisi katika wimbo huo na kusema kuwa maafisa wa polisi wanaodhani aliwaponza wanakosea.



Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia chombo cha habari KHOU11 kuwa hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa ikizama katikamafuriko.

“Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni kinyume na maafisa wa polisi,” aliongeza.

Mnamo mwezi Aprili, Beyonce aliambia jarida la Elle kwamba anaheshimu polisi lakini hapendi unyanyasaji.



Beyonce alisema “Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi anakosa kwa sababu.”

“Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi pamoja na familia za maafisa hao ambao hujitolea ili kuhakikisha tuko salama,” aliongeza.


Pengo la samata bado lipo TP Mazembe

Mshambuliaji wa kimataifa Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba kwa sasa pengo la Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta linaonekana TP Mazembe.



Ulimwengu akiongea na Clouds FM alisema TP Mazembe kwa sasa inamkosa mshambuliaji mwepesi, mwenye uwezo wa kufunga kama Samatta.

Samatta ameondoka timu hiyo ya DRC Januari mwaka huu baada ya kushinda nayo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anakoendelea vizuri hivi sasa.

Tangu kuondoka kwa Samatta, Mazembe imeonekana kupoteza makali yake kiasi cha kuvuliwa mapema ubingwa wa Afrika.

Mazembe ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kombe la Shirikisho.

Katika mechi iliyopita Mazembe ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Stade Gabesien Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.

Ulimwengu aliyecheza kwa dakika 45 juzi kabla ya kutoka uwanjani akiwa anachechemea, alisema timu kwa sasa haina mtaalamu wa kufunga mabao kama alivyokuwa Samatta.

“Pengo la Samatta linaanza kuonekana sasa, pale mbele hakuna na anayeweza kufunga kama Samatta, tunapoteza nafasi nyingi sana, hilo ndilo tatizo,”amesema Ulimwengu.

Sasa Mazembe itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ikitakiwa kwenda kuulinda ushindi huo mwembamba nchini Tunisia

mwanamke aunda boti yenye umbo la uke wake

Mahakama moja ya Japan imemwachia huru mwanamke mmoja aliyetengeza boti iliyofanana na uke wake.


Jaji aliamuru kwamba boti ya Megumi Igarashi iliofanana na uke wake na yenye rangi nyingi haikuashiria umbo la uke.

Hatahivyo ,alipigwa faini ya dola 3,700 baada ya jaji kuamuru hakuvunja sheria kwa kusambaza data ya uke wake ambayo inaweza kutumika kutengeza umbo la uke wake.

Sheria kali za Japan zinapinga kuonyeshwa hadharini kwa sehemu za siri.

Igarashi mwenye umri wa miaka 42, kwa jina Rokudenashiko au ”good for nothing girl” alikamatwa mwaka 2014 baada ya boti yake kuonyeshwa katika duka moja la vifaa vya ngono mjini Tokyo.

Alishtakiwa chini ya sheria ya mambo machafu kwa kuonyesha boti hiyo na kusambaza data yake kwa wale waliochangisha fedha ili itengezwe.

Siku ya Jumatatu jaji mmoja aliamua kwamba rangi zake zinazong’aa na mapambo yake hayaonyeshi ukweli wa umbo la uke.

“Lakini data yake licha ya kutokuwa na umbo la uke itatumika kutengeza uke wa Bi Igarashi kwa kutumia 3D na hivyobasi ni uchafu,” alisema jaji.

Bi Igarashi alipigwa faini nusu ya Yen 800,000 zilizohitajika na afisi ya mashtaka

Tuesday, 10 May 2016

 Ommy Dimpoz hapendi kuwa na uhusiano na staa mwenzie kwasababu anaamini kuwa hatokuwa huru. Hata hivyo amewataja Mamiss Tanzania wawili ambao anasema kama wangekuwa sio mastaa basi lazima angetupa karata zake.



“Unakuwa hauna privacy,” ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.


“Sometime unaishi sio maisha yako, unataka uishi kwa kuwaridhisha mashabiki wa girlfriend wako kwasababu ukifanya hivi watatukana, hawajui labda na wewe uliumizwa sehemu gani, kwahiyo. Sometimes inakuwa sio feelings zako, ni feelings za mashabiki wa girlfriend wako, sasa hiyo inakuwa haijakaa vizuri,” ameongeza.

“Staa ambaye asingekuwa staa ningetamani kudate naye labda Wema, wengine siwezi kuwataja ni wake za watu. Kuna mwingine siwezi kumtaja sababu ameolewa, ni staa alikuwa Miss.”

Wema Sepetu akipiga mabusu ya ukweli kwenye hii movie

Ukiwa muigizaji kubali yote. Kuna scenes ambazo zitakuhitaji upigane busu na mtu anayecheza kama mpenzi wako na ili kupata uhalisia wa tukio huna budi kubadilishana mate kwenye screen.



Wema Sepetu hana kinga ya ukweli huo na ndio maana kwenye clip iliyowekwa Instagram, anaonekana akibusu na muigizaji mchanga, Koko Byanko utadhani kweli ni wapenzi.

Moze iyobo na Aunty Ezekiel kupata mtoto wa pili

Wakati mtoto wa Aunt Ezekiel na Mose Iyobo akikaribia kutimiza mwaka mmoja hivi karibuni, Mose amefunguka kuhusu kupata mtoto mwingine wakiume na mrembo huyo kutoka kiwanda cha filamu.


Akizungumza na Bongo5, Mose amesema kwa sasa anafurahia maisha na mrembo huyo wa filamu na soon watapata mtoto mwingine wakiume.

“Sasa mimi na Mama Cookie tunamipango endelevu, kama hivyo ushamuona Cookie bado kuna kaka yake Cookie anakuja na vitu vingine vitaendelea, soon mtasikia tu,” alisema Mose.

Mose alisema anafuraha kuwa kwenye mahusiano na Aunt Ezekiel

Ugomvi wa Jaguar na Akothee kinachoendelea

Meneja wa msanii wa Kenya, Akothee amemjibu Jaguar baada ya kumuingiza msanii wake kwenye ugomvi wao na Prezzo.



Akifanya mahojiano na Kiss FM, Jaguar alisema, “so mi ntaachia Shaffie hio job aongee na yeye kwa sababu Prezzo ni mdifficult, tunaweza enda studio tena aanze mavitu haziko. Unajua ni male version ya Akothee.”

Kutokana na kauli hiyo meneja wa Akothee ameimbia edaily kuwa, “Akothee is very busy right now. She is working on projects with top South African artistes, among other regional and international musicians. Most of the time she is not in Kenya as she is building her brand appeal.”

Aliongeza kuwa, “We are not even aware that Jaguar called her a ‘socialite’. That tells you how busy she and the team are. Akothee is too busy to engage Jaguar in cheap publicity stunts.”

Saturday, 7 May 2016

Gigy Money ; sipendi kufanya mapenzi

Video queen ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa yeye siyo mtu wa kupenda kufanya mapenzi kama watu wanavyodhani.


Akizungumza na Bongo5, Gigy amesema maisha aliyopitia yamemfanya awe ni mwanamke asiyependa kufanya mapenzi.

“Mimi nimepoteza ile ari ya kufanya mapenzi au kuwa na mpenzi mmoja au nijiachie na mwanaume kama mtu na mpenzi wake siwezi, sasa hivi natafuta maisha, pesa mbele,” alisema Gigy. “Kama yeye ana wivu na mimi, mimi sina wivu na mwanaume,”

Gigy amesema taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba anajiuza siyo za kweli, kwani yeye ana mwanaume ambaye anamuudumia kila kitu ingawa hawafanyi mapenzi.

“Nina mtu ambaye ananihudumia, ananipa mtaji ya biashara zangu. Pia hata kwenye muziki anawekeza pesa yake. Kwa hiyo waache wanifikie hivyo wanavyofikiria, mimi nafikiria navyojijua, mimi nipo tofauti sana na wanavyozungumza, ukijaribu kukaa na watu wangu wa karibu watakwambia,” alisema Gigy.

Fifa kuifungia club ya Simba

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.


Rais wa FIFA, Gianni Infantino

Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.

Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.

Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.

Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.

Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.

FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.

Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.